Na Mwandishi wetu

Akizungumzia maadhimisho hayo Dr Asser Mchomvu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki anasema kuwa uongozi wa KH unapenda kuwashukuru wadau wote walioshirikiana nao katika kuiwezesha KH kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wote.
indexMkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki,Dk.Asser Mchomvu .
Dr Mchomvu anaongeza kuwa katika kutambua mchango wa wadau mbalimbali kwa kufikisha miaka 29, KH itafanya maadhimisho yake kwa kutoa msaada kwa vituo vya afya pia kufanya upimaji wa kinywa na meno bure. “Madhimisho haya yataambatana na utoaji wa vifaa katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha, ambapo KH itatoa msaada wa vitanda vya hospitali na magodoro siku ya Alhamis tarehe 17.03.2016,” alisema Dr Mchomvu Alisisitiza kuwa pamoja na hilo, KH itatoa pia huduma ya upimaji na ushauri wa afya ya kinywa na meno kwa wananchi kwa siku mbili bure ( siku ya Jumatano na Alhamis tarehe 16 na 17, Machi 2016) kuanzia saa 2 asubuhi, pale pale Hospitali ya KAIRUKI, Mikocheni, Dar es Salaam.
KAI1 KAI2
Dr Mchomvu anaeleza kuwa, kutakuwa na ghafla fupi ambapo Mkurugenzi atatoa salamu baada ya kukata keki na watoto waliozaliwa KH mwaka 1987. Watu wote wanakaribishwa katika ghafla hiyo itakayofanyika hapo KH siku hiyo ya Alhamisi tarehe 17.03.2016 saa 10 jioni.

Kwa upande mwingine KH imekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma zake huku ikizingatia ufanisi na ubora katika utowaji wa huduma zake kwani inatumia vifaa vya kisasa ambavyo vina ubora wa hali ya juu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...