Kampuni ya Dhahabu ya Geita(GGM) imeshiriki
maonyesho ya usalama na afya mahala pa
kazi kwenye viwanja vya Jamhuri mjini
Dodoma.Maonyesho hayo yameratibiwa na wakala wa usalama na Afya mahala pa
kazi(OSHA) kuelekea maadhimisho ya siku ya usalama na afya mahala pa kazi Duniani.
Akizungumza
kuhusu ushiriki wa Geita Gold Mine(GGM) kwenye maonyesho hayo,Ofisa mawasiliano
mwandamizi wa Geita Gold Mine(GGM) Bw
Theophil Pima amesema kuwa kampuni ya GGM ni mdau wa usalama na afya mahala pa
kazi na ndiyo sababu ya kushiriki
maonesho hayo.
“GGM inatambua usalama ni kitu muhimu kuliko
hata uzalishaji na ndiyo maana imeshaweka tamko kabisa kuwa Usalama ndicho
kipaumbele chake kikubwa kuliko vyote katika shughuli zake.Tumekuwa tukishirikiana
kwa ukaribu na wakala wa usalama na afya mahala pa kazi na kupatiwa vyeti
mbalimbali”alisema Bw Theophil Pima na kuongeza kuwa wafanyakazi wote wa GGM kabla ya kuanza kazi hupatiwa mafunzo maalumu
ya usalama mahala pa kazi ili kuepusha ajali ambazo ni changamoto kubwa kwa
migodi mingi Duniani.
Akizungumzia kauli mbiu ya maonesho hayo kuwa "Msongo wa mawazo mahala pa kazi ni
changamoto yetu sote", Bw Theophil Pima amesema kuwa Kampuni ya GGM kama
zilivyo kampuni zingine inayo changamoto ya baadhi ya wafanyakazi wake kuwa na
tatizo la msongo wa mawazo na ndiyo maana wanayo program maalumu ya kuleta
madaktari bingwa kutoa ushauri na utaalamu wa kisaikolojia kwenye hospitali yao
hapo mgodini.
“Msongo wa mawazo ni changamoto kubwa kwa
sababu husababisha mfanyakazi awe na mawazo na kushindwa kufanya kazi kwa
ufanisi.Wakati mwingine msongo wa mawazo hasa kwa wataalamu wanaoendesha
mashine migodini unaweza kusababisha ajali”alisema Bw Theophil Pima na kuwaomba
watanzania mkoani Dodoma wajitokeze kwa wingi kwenye banda lao ili kuona vifaa
vya kisasa vinavyotumika kwenye masuala ya afya na usalama kwenye kampuni yao.
Akizungumzia maonyesho hayo Mkurugenzi wa usalama na afya kutoka wakala wa usalama
na Afya mahala pa kazi(OSHA) Mhandisi Alex Ngata amesema maonyesho kama hayo ni
fursa ya kutoa mafunzo kwa waajiri na
wafanya kazi ili watambue nafasi ya afya na usalama mahala pa kazi na namna ya
kukabiliana na chngamoto mbalimbali ukiwemo msongo wa mawazo.
Afisa mawasiliano mwandamizi wa Kampuni
ya Geita Gold Mine(GGM) Bw Theophil Pima akizungumza na vyombo vya habari
kwenye maonesho ya usalama na afya mahala pa kazi.Pembeni yake ni Afisa
Utumishi wa GGM Bw Joseph Mgire(wa kwanza kushoto) na Bw Chacha Magige ambaye
ni mratibu wa masuala ya usalama mahala pa kazi GMM.Wengine ni wataalamu kutoka
GGM.
Wakazi
wa Dodoma wakitembelea banda la maonyesho la Geita Gold Mine
Bw Mohamed Mwaimu(katikati)kutoka
kitengo cha dharura na uokoaji cha GGM akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya
msingi waliotembelea banda la Geita Gold Mine jinsi ya kumuokoa mtu aliyepata
ajali ya kumwagikiwa kemikali mgodini.
Mtaalamu wa afya mahala pa kazi Bw Shija Ayoub akionyesha upimaji wa
kelele na vumbi kazini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...