Kufuatia wadau wengi kuhitaji kujua hatua zitakazochukuliwa na Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) dhidi ya hukumu ya kesi ya rushwa Na. 75/2014
iliyokuwa ikimkabili Bw. William Mhando aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) na wenzake watano.
TAKUKURU inapenda kuufahamisha umma
kwamba inafanya taratibu za kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo iliyosomwa tarehe 14/4/2016 na
Mhe. Hakimu Mkazi Hellen katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaniaba ya Hakimu
Mkazi Mkuu Mhe. Kyey Rusema. Katika hukumu hiyo washtakiwa wote sita (6) waliachiwa
huru.
Aidha, TAKUKURU inawataka wadau na wananchi kwa ujumla kutambua kwamba ni utaratibu
wa kisheria kwamba upande usioridhika na hukumu iliyotolewa kukata rufaa katika Mahakama
ya juu.
Baadhi ya mahakimu hawajaisoma namba bado. Kesi ya wizi wa wazi wazi wa taasisi ya umma na matumizi mabaya ya madaraka ameachiwa kabisaa? Kweli Magufuli anakazi na tumwombee. Alex bura dar.
ReplyDeleteJaji mkuu wa Tanzania tunaomba uwaangalie kwa jicho la 3 baazi ya mahakimu coz baazi ya maamuzi ya mahakimu tuna mashaka nayo coz haiingii AKILINI serikali ina pambana kuitokomeza rushwa lakini upande wa mahakama zetu bado kama hawajui nini madhara ya RUSHWA na tujiulize why serikali inakua I nashindwa kesi zikifika mahakamani? hapo pana jambo si bule
ReplyDelete