Wakazi wa Mlandizi mkoa wa pwani na vitongoji vyake,Wamerahisishiwa jinsi ya kupata huduma mbalimbali za huduma za mawasiliano kwa kuzinduliwa kwa duka jipya na la kisasa la Vodacom Tanzania lililozinduliwa leo ukiwa ni mkakati uliowekwa na kampuni hiyo kwa kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi nchini kote.Mwaka huu kampuni hiyo imedhamiria kufungua vituo vipatavyo 500 nchini kote.
Kituo hiki kipya kinatarajia kutoa huduma kwa wateja wa Vodacom wanaoishi Mlandizi na vitongoji jirani ambao walikuwa wanatembea mwendo mrefu kufuata huduma pia kitahudumia wasafiri mbalimbali wanaotumia barabara ya morogoro.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,Hassan Saleh amesema kuwa mkakati huu wa kufungua vituo vya kutoa huduma za Vodacom umebuniwa ili kuwapunguza wateja adha ya kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma.
“Kwetu Vodacom wateja wetu ni wafalme na tunasikiliza ushauri wao,pamoja na kuwa na maduka sehemu mbalimbali lakini bado tumeona kuna haja ya kuwasogezea zaidi huduma wateja wazipate popote pale walipo na kwa wakati wowote”.Alisema.
Aliongeza kuwa kupitia huduma hii ya vituo vya mauzo kampuni itazidi kupanua wigo wa ajira nchini kwa kuwa watanzania zaidi ya 1000 watanufaika na mpango huu na ni utekelezaji wa moja ya malengo ya kampuni ambayo ni kufanya uwekezaji wenye mwelekeo wa kuwanufaisha watanzania.
Akifungua kituo hicho kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Pwani, Kaimu Katibu tawala wa Wilaya hiyo,Anathory Mhango aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kusambaza huduma zake karibu na wateja na aliwataka wakazi wa Mlandizi kutumia huduma za mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha maisha.
Mmoja wa wakazi wa Mlandizi Sheikh Daruwesh Mohamed Luhanjo akiongea kwa niaba ya wakazi wenzake alisema kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kutawapunguzia kero wakazi wa eneo hilo kutembea umbali mrefu kufuata huduma za Vodacom “Tunashakuru Vodacom kwa kutukumbuka wana Mlandizi”alisema
Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya
Kibaha,Anathory Mhango(watatu kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akikata
utepe kuzindua duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo Mlandizi
Mkoa wa Pwani,Wengine kutoka kushoto Meneja wa duka hilo,Godfrey Lyimo,Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja
Vodacom,Brigita Stephen na Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi.
Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani,Anathory Mhango(wapili kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo na Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom Tanzania,Brigita Stephen(kushoto)wakimshuhudia Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi(kulia)akimsajilia namba za simu mteja wa kwanza Janeth Mnzava wakati wa uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo”Service desk” lililopo Mlandizi.
Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha,Anathory Mhango(wapili kushoto) kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akigonganisha glasi na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati wa uzindua wa duka jipya la kampuni hiyo”Service desk” lililopo Mlandizi.
Kaimu Katibu tawala wa Wilaya ya
Kibaha,Anathory Mhango(wapili kushoto)kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo akikata
keki kuashiria uzindua wa duka jipya la Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo
Mlandizi Mkoa wa Pwani,Wengine kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom,Brigita
Stephen na Meneja Mauzo wa kanda hiyo,James Kigodi.
Mkazi wa Mlandizi Wilaya ya Kibaha Mkoa wa
Pwani,Darueshi Luwanja akilishwa keki na Kaimu Katibu tawala wa Wilaya hiyo,Anathory
Mhango kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo,wakati wa uzinduzi wa duka jipya la
Vodacom Tanzania”Service desk” lililopo Mlandizi,Wengine kutoka kushoto,Meneja
Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu,Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja Vodacom,Brigita
Stephen na Mkazi wa eneo hilo Abdallah Ahmed.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...