Wanafunzi 42 wa mwaka wa tatu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini, wakiambatana na wahadhiri wao walipata fursa ya kutembelea migodi ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na kampuni ya uchimbaji ya Acacia.

Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyofanyika tarehe 11 na 12 mwezi huu, wanafunzi hao pamoja na wahadhiri wao walijionea shughuli za uchimbaji wa madini wa chini ya ardhi katika Mgodi wa Bulyanhulu (Underground mining) na uchimbaji wa juu wa ardhi (Open pit mining) katika Mgodi wa Buzwagi. Wanafunzi hao vilevile walipata fursa ya kujifunza namna ya uchenjuaji wa dhahabu katika migodi yote miwili.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia ina Mkataba wa Makubaliano (MoU) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kama sehemu ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii. Katika makubaliano hayo Acacia hufadhili ziara za mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea fani za Uhandisi Migodi na Uhandisi Uchenjuaji Madini kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam kwa mwaka mara moja na kutoa fursa kwa wanafunzi hao ya kujifunza kwa vitendo kwa muda wa miezi miwili kila mwaka katika migodi yake.

Kampuni ya Migodi ya Acacia ndio kampuni kubwa zaidi ya uchimbaji wa dhahabu nchini na inamiliki migodi mitatu ya Buzwagi na Bulyanhulu iliopo katika wilaya ya Kahama Shinyanga na ule wa North Mara uliopo Nyamongo mkoa wa Mara.
Kundi la wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakielekea chini ya mgodi.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakiwa katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakimsikiliza kwa makini Afisa Mafunzo wa Mgodi huo, Caroly Chundu wakati akitoa maelezo kuhusu maswala ya usalama kabla ya kuingia mgodini
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salam wakipata maelezo kutoka kwa Amos Mokoge, Mtaalam wa uchenjuaji katika kinu cha Uchenjuaji dhahabu kuhusu motor ya kinu cha Uchenjuaji wa dhahabu.
Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Migodi Karim Mleli katika bwawa la tope visusu ambalo linatumika kuhifadhi maji yanayotoka kwenye mtambo wa kuchenjulia dhahabu katika mgodi wa Buzwagi.
Wanafunzi waliotembelea Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa wa mgodi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...