Na Baltazar Mashaka, MWANZA

WAUMINI wa dini ya Kiislamu nchini wameaswa kurejesha imani ya dini ya uislamu kama ilivyokuwa zamani na kuepukana na zile zinazohamasisha mauaji ambapo ni kinyume na imani ya dini hiyo zaidi wamewatakiwa kuhimiza upendo na amani miongoni mwao  na kulaani  mauaji ya kinyama yaliyotokea hivi karibuni na kuiomba serikali iwasake wahusika hata kama ni waislamu waliofanya kitendo hicho ili sheria ichukue mkondo wake, na kuhoji ni uislamu gani wa chuki usiovumilia na kutotambua haki ya mtu ya kuishi ikiwa Mtume Muhammad (S.A.W) ameweza kuihurumia miti isikatwe kwani nayo ni haki ya kibinadamu.


Kauli hiyo imetolewa juzi na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke wakati wa dua maalmu iliyondaaliwa na Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania ya kuwaombea waumini watatu waliouawa kwa kuchinjwa msikitini na kundi la watu wasiofahamika wakati wakiswali.
Waumini hao walivamiwa Mei 18, mwaka huu majira ya saa 2:00 wakiwa kwenye msikiti wa  Rahman uliopo Ibanda Relini wakiwa katika rakaa ya tatu kabla ya taa kuzimwa na wauaji hao na kuwaamuru kulala kifudikifudi ambapo wakamkamata Imamu wa msikiti huo, Feruz Ismail na kumchinja shingo kutokea kisogoni na kisha kujeruhi mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 13.

“Hakuna mtu ameyafurahia mauaji hayo ambayo yametufedhehesha mkoa wa Mwanza na leo sifa yetu imetiwa doa na watu wachache kwa maslahi yao wanayofahamu wao wenyewe. Tumedhalilika na kuchezewa sababu tumeacha uislamu wetu wa asili,"amesema Kabeke. Mauaji hayo ya kinyama yamewadhalilisha Waislamu na Watanzania wote ambayo yameuingiza Uislamu kwenye matatizo makubwa na kuwataka waumini wa dini hiyo kurejea kwenye uislamu wa asili wa imani ya dini yao.

“ Dini yetu imevamiwa na kuingizwa kwenye mambo yasiyofaa,hatusemi ni waislamu ama ni wakristo bali mazingira yanatuliza na kinachotuumiza ni mtu kuchinjwa kutokea nyuma kwenda mbele, inaumiza na inauma sana. Machozi tunayoyatoa leo yatubadilishe yawe daftari na kalamu na yaturudishe kwenye uislamu wa asili yetu,” amesema Sheikh Kabeke.

Aidha, ameeleza kuwa dua zinasomwa sehemu mbalimbali zitatoa majibu na kuiomba serikali na vyombo vyake kutowadhuru waislamu bali wafanye kazi yao kwa weledi wakizingatia taaluma yao kuwabaini wahalifu hao na kuomba ulinzi kwenye nyumba za ibada ili kukabiliana na vitendo aina hiyo. 

Mbali na dua hiyo baadhi ya wahanga walionusurika kuuawa Abeid Ghati amesimulia tukio hilo la kinyama lakini akashindwa kuendelea na kujikuta akiangua kilio na kuzua simanzi kwa umati wa waumini waliojitokeza kwenye dua hiyo ambapo taasisi ya Bilal Muslim imeweza kutoa ubani kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na mtoto aliyenusurika kuuawa katika tukio hilo ambapo amejeruhiwa katika sikio la kushoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...