Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.

SERIKALI ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.Rais Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa Viwanda.

Wakati Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo hilo.

Abdallah Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo kuwa na viwanda.

Anasema kuwa lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi haya kwani wameahidi hivyo lazima watende. Ulega anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.

Anasema kuwa kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda. “Kimsingi jimbo langu la Mkuranga ni kubwa kama nilivyosema na uzuri zaidi lina ardhi nzuri sana na ndiyo maana naomba wahisani na wawekezaji wa ndani kujitokeza kuja Kuwekeza na zaidi kijenga viwanda.”anasema ulega.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...