Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye Uwanja wa Kololo jijini Kampala kuhudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Mwinyi alihudhuria pia sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Rais Mstaafu Kikwete pia alihudhuria sherehe za uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi wa mataifa mbalimbali katika viwanja vya Kololo jijini Kampala.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa viongozi wa dini wa Taifa la Uganda katika viwanja vya Kololo jijini Kampala. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo kwa furaha na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Kololo jijini Kampala Uganda. Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 13, 2016

    Bila shaka sherehe za kumwapisha Mh. Rais K. Mseveni zimekwisha salama. Sasa unarejea Tanzania. Nichukue nafasi hii kutoa ushauri. Kumetokea mkanganyiko usio wa lazima katika suala zima la kushughulikia shida ya sukari. Viongozi wengi sasa wameenda beyond expetations. Wameanza kuzuia kiholela sukari isiuzwe. Wameanza kukamata hata wale wenye kilo 350 tu. Hizi ni vurugu zinazolitia doa kubwa serikali yako. Heshima uliyoijenga sasa itaanza kupotea. Nafikiri kuna vyombo vya dola ambavyo vinaweza kufanyakazi kwa umakini. Hivyo ndivyo vifanye kazi hiyo tena kimya kimya. Tulioangalia taarifa ya habari leo (12.05.2016) ya ITV tumefadhaika kwa tuliyoyaona na kusikia. Sasa ni vurugu tupu. Hii ni hatari sana kwa heshima ya kiti cha Rais. Kinachoonekana wazi ni vurugu za viongozi kuanza kuwanyanyasa watu wasiohusika na hujuma. Ombi langu. Umerejea nchini kutoka Uganda sasa waambie viongozi watulie. Waache kuutia doa uongozi wako. Kama ni kuagiza sukari iagizwe ya kutosha wakati huo viwanda vikijipanga kwa uzalushaji wa uhakika. Nakutakia utawala mwema uliotukuka. Lakini uongozi wako umetiwa doa ambalo sikutegemea litokee ghafula baada ya kazi nzuri uliyoifanya.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 13, 2016

    Wanamajungu wanadai kuna uhasama kati ya Uhuru na JPM, hebu dekishia kwenye picha walivyo peace. Issue ya bomba la mafuta was up for a grab. Mwenye mwenye kisu kikali sharp shooter John Joseph Pombe Magufuli ndo akala mnofu. Nothing personal there kila mtu alikuwa kimaslahi ya nchi anayoongoza, Mungu mkubwa rais wetu mpendwa akamgalagaza Uhuru. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki JPM

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...