MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz  amezindua rasmi Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’  na kuwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku msanii Rich Mavoko akisaini mkataba wa kufanya kazi na Lebo hiyo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. 

WCB inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Tanzania kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamuziki, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WCB, Diamond Platinumz alisema lengo la kuanzishwa lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sanaa ya muziki izalishe pato la taifa.

Msanii Diamond ameomba serikali kuwaunga mkono ili waweze kusonga mbele maana kwa sasa amekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakimtegemea katika kufanya sanaa ya muziki.
 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz (wa pili kushoto) akiwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo ya ‘WCB Record Label’ ambayo ameizindua leo ndani ya hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza pamoja na mameneja wake Hamis Tale na Mkubwa Fela. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Msanii Queen Darleen, Raymond na Hamonize. 
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akisaini mkataba wa kufanya kazi na msanii Rich Mavoko huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo. Nyuma ni uongozi wa WCB na msanii Diamond.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akibadilishana mkataba na Rich Mavoko mara baada ya kusaini huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2016

    Asante sana#simbaaaaaaaa karibu sana WCB Wasafi MAVOKO hapa kazi 2 Majungu kwa Ali na Sepetu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2016

    SASA MTAFUTE WASANII WENYE SAUTI TOFAUTI MAANA WOTEJ1 NYIE SAUTI ZENU ZINAFANANA SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...