Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
SHIRIKISHO la mpira wa Miguu Nchini(TFF) kuanza kusimamia rasmi mechi zote za kimataifa zitakazofanyika hapa nchini, Kuanzia sasa TFF itahusika na kuratibu mechi hizo, kusimamia mapokezi ya timu, usalama wao, sehemu za kufikia, viingilio pamoja na uuzwaji wa tiketi za mchezo husika na maamuzi hayo ni kama yamekuja baada ya Yanga kuruhusu wapenzi wa soka nchini kuingia bure katika mchezo wao dhidi ya TP Mazembe hali iliyozua tafrani.

Katika mchezo huo vyombo vya usalama vilipata wakati mgumu kuzuia mashabiki wa timu hiyo baada ya kutaka kuingia uwanjani ikiwa tayari ulikuwa umejaa na Vurugu hizo ziliwalazimu wanausalama kutumia mabomu ya machozi pamoja na maji ya kuwasha ili kuwatawanya mashabiki hao waliofikia hadi hatua ya kuangusha moja ya geti la uwanjani hapo.

Kwa mujibu wa kanuni ya FIFA kifungu cha 67, CAF kifungu cha 59 na TFF kifungu cha 52 kinalipa mamlaka shirikisho husika kusimamia kila kitu ikiwemo maandalizi ya machezo, mapato, matangazo na vingine muhimu katika mchezo huo namba 107 wa Yanga dhidi ya Mazembe Yanga walishapanga viingilio lakini walibadili maamuzi na kuamua kuingiza watu bure na kurusiwa na CAF kwa masharti ya kuingiza mashabiki elfu 40 tu lakini walizidi hadi 60 elfu.

Pia TFF kupitia kwa Wizara yenye dhamana iliruhusu mchezo huo lakini nayo ikitoa masharti ya kutoharibu miundombinu ya uwanja, kulipa gharama za uwanja, gharama za CAF pamoja na TRA na walikubaliana na kwa sasa wanafanya mawasiliano na watu wa Wizara, CAF na TRA kujua Yanga wanatakiwa kulipa kiasi gani. 

Pia kunasubiriwa ripoti kutoka CAF juu ya matukio ya ndani na nje ya uwanja yaliyojitokeza katika mchezo huo dhidi ya Mazembe na zaidi TFF wanaitakia Yanga kila la kheri kuelekea katika mechi zake zilizobaki kwani matokeo ya mchezo kati ya Mo Bejaia na Medeama yanaipa Yanga matumaini ya kusonga mbele endapo watafanya vizuri katika mechi zake zilizobaki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MEDEAMA wataishia kujitoa endapo hawatapewa mgao wao wa dola za kimarekani 150,000. Rais wa klabu hiyo Armah MOSES amekaririwa akisema hivyo jana kabla ya mchuano wao na MO Bejaja huko Sekondi, Ghana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...