WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) watembelea chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na kuzindua Jumuiya ya wanafunzi wa kodi Vyuoni katika chuo hicho jijini Dar es Salaam leo.


Akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema kuwa jumuiya hiyo ni kwaajili ya kukuza ufahamu wa maswala mbalimbali ya kodi kwa wanajumuiya katika chuo cha IFM pamoja na wasio nanajumuiya.

amesema kupita wanachama wa jumuiya ya wanachuo hicho wawe ni chachu ya kuongeza ari wa jamii kupenda kulipa kodi kwa hiari na ni njia pekee ya kuwafikia wananchi wengi na kuibuliwa kwa vyano mbalimbali vya kodi.

Kayombo amewaasa wanafunzi wa jumuiya ya kodi vyuoni kuwa mawakala wazuri pindi wanaponunua bidhaa mbalimbali katika maduka kwa kudai lisiti au kuwakumbusha wauzaji kutoa lisiti kwa wateja wao, na wateja wahakikishe lisiti iliyotolewa kama ni ya tarehe husika.
Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) katika ufunguzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa Kodi Vyuoni jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa jumuiya wa wanafunzi wa Kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha (IFM), Amos Ojode akizungumza na kuwashukuru wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuwapa nafasi wanafunzi wa chuo cho kujifunza na kuzindua jumuiya ya wafunzi wa kaodi vyuoni katika chuo chao.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) wakiwa katika uzinduzi wa Jumuiya ya wanafunzi wa kodi katika chuo chao jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...