NA RAMADHANI JUMA
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imefanikiwa kukusanya asilimia 80.28 ya
mapato kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya ndani katika mwaka wa fedha
2015/2016 uliomalizika Juni 30 mwaka huu.
Katika mwaka huo wa fedha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ilipanga
kukusanya shilingi 4,566,075,181 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani (own
sources) ambapo mpaka mwisho wa mwaka huo makusanyo halisi ni 3,665,699,279
sawa na asilimia 80.28 ya makisio.
Akizungumza katika kikao cha mwaka cha Baraza la Halmashauri ya Manispaa hiyo,
Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Jaffar Mwanyemba aliwaambia wajumbe wa
Baraza hilo kuwa, mafanikio hayo yametokana na uchapaji kazi wa watendaji na
madiwani wa Manispaa hiyo.
Katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa, Mstahiki
Mwanyemba aliwapongeza wote waliohusika kwa namna yeyote katika kufikia hatua
hiyo huku akitoa wito kwa Ofisi ya Mkurugenzi na Madiwani wa kuimarishwa kwa
juhudi zaidi katika ukusanyaji katika mwaka wa fedha 2016/2017.
"Mwaka mpya wa fedha umeshaanza hivyo Mkurugenzi na watendaji wako anzeni
kukusanya kodi mapema...na waheshimiwa madiwani tuongeze nguvu katika
kusimamia vyanzo vya mapato katika maeneo yetu" alisema.
Aidha, katika mkutano huo ambao kwa mujibu wa kanuni unakuwa na ajenda mbili tu
ambazo ni kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka
uliopita na kupitia na kupitisha ratiba ya vikao vya Halamshauri kwa mwaka
unaofuata, wajumbe walipitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...