Kundi la watoto yatima wanaotunzwa na Karrima na wahisani wenzake Waingereza kutoka Norwich hapa Uingereza
Baadhi ya wahisani kutoka Norwich wakiwa katika halfa ya utoaji misaada kwa kituo cha kulea yatima, Bagamoyo


Mwanadada wa Kitanzania, Karrima Carter, mwenye makazi yake Norwich, hapa Uingereza, wiki hii ameshirikiana na wahisani wenzake kutoka Uingereza kutoa misaada kwenye kituo cha kulelea watoto yatima huko Bagamoyo na uzinduzi wa vyoo vilivyokarabatiwa kwa uhisani wa dada huyo na wahisani wenzake kutoka Uingereza.
Tukio la kwanza lilifanyika Jumapili iliyopita na kuhudhuriwa na baadhi ya wasanii mbalimbali kama vile Gabo na Faiza Ally (ambao walialikwa rasmi kwa minajili ya kuwapa tabasamu watoto yatima), na tukio la pili lilifanyika Jumatatu iliyopita.
Picha na maelezo ya tukio la tatu la kukabidhi madawati zitawajia kesho. Awali, Karrima alisita kuhusu wazo la ku-blogu kuhusu matukio haya akisema kwamba asingependa 'publicity' lakini mie binafsi nilimshauri kuwa kuweka hadharani habari hizi kunaweza kusaidia kuwahamasisha Watanzania kuhusu utamaduni wa kutoa misaada kwa wenzetu wenye uhitaji, eneo ambalo ni maarufu hapa Uingereza lakini ni geni kwa nchi nyingi za Afrika.
Karrima amekuwa akijibidiisha katika sekta hiyo ya misaada kwa wenye uhitaji kwa kitambo sasa. na amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kwa wakazi wenzie wa Norwich.

Karrima n wahisani wenzake kutoka Norwich, uingereza, mara baada ya kuwasili nchini Tanzania kwa hafla mbalimbali za utoaji misaada.
Hafla ya kuzindua vyoo katika Shule ya Msingi Ilala, ambavyo vilifanyiwa ukarabati kwa uhisani wa Karrima na wenzie kutoka Norwich, Uingereza

Karrima na wahisani wenzie kutoka Norwich wakiwa shuleni Ilala.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...