Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.

Aidha, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60 kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi wanalima mazao hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi  na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah .
Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa(hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kutoka  kushoto), Mhe. Tano Mwera (Busega),Mhe. Joseph Chilongani(Meatu), Mhe. Benson Kilangi (Itilima ) na Mhe. Seif Shekalaghe.Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa waSimiyu, Ndg. Jeremia Shigala akichangia katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu .
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...