Mkuu mpya wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiongea na wadau mbalimbali waliouthuria katika sherehe za kuapishwa kwa wakuu wa wilaya wapya wa wilaya tano zilizopo mkoa ndani ya mkoa wa Arusha ,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwataka wadau mbalimbali pamoja na wananchi kumpa ushirikiano katika kufanya kazi ,huku akisisitiza kuwa swala ya siasa pamoja na mambo ya kisiasa yameisha sasa hivi ni muda wa kufanya kazi tu(Habari picha na Woinde Shizza, Arusha )
 Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha walioapishwa Jumamosi  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Felexs Ntebenda pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. Adolfu Mapunda nje ya jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa
Mkuu wa wilaya ya Longido   Daniel Geofrey Chongolo akikaribishwa rasmi na  mmoja wa viongozi wa CCM  wilayani humo kwa kupewa shuka la Kimasai hii ikiwa ishara ya kuwa wilaya yake ina wananchi wengi wa kabila la kimasai na Kiarusha ambao ni wafugaji
 Aliekuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Wilson Nkambaku akiongea na wananchi wa mkoa wa arusha pamoja na baadhi ya viongozi wakati wa sherehe za kuwaapisha  wakuu wapya wa wilaya ambao wameteuliwa na rais Magufuli,ambapo mkuu huyu wa wilaya aliwaomba wananchi pamoja na wafanyakazi wa serekali kuwapa ushirikiano wa kutosha viongozi walioteuliwa huku akimshukuru rais magufuli kwa kumpa ushirikiano katika kipindi cha miezi nane aliyefanya nae kazi huku akimuaidi kuendelea kutoa ushirikiano katika serekali yake pamoja na chama  kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...