Meneja Mkuu wa Efm  Bw. Denis  Ssebo akizungumza leo na waandishi wa habari  juu ya tamasha kali  la kila mwaka lijulikanalo kama MUZIKI MNENE  ambalo litaanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko  jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom Bi.  Nandi Mwiyombella akizungumza leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon  jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).

REDIO ya burudani ya Efm imezindua tamasha la kila mwaka lijulikanalo kwa jina la MUZIKI MNENE,ambalo linatarajia kuanza rasmi Agosti 28  mwaka huu katika eneo la Boko.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Mkuu wa Efm, Denis  Ssebo amesema tamasha hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki 12 sawa na miezi mitatu ambapo muziki utapigwa  katika bar 12 za vijijini vya Dar es Salaam na  Pwani ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Tunasepa na kijiji '.

Alisema mziki mnene mwaka huu itaenda sambamba na kampeni ya nje ndani ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku nne mfululizo.
Ssebo alivitaja vipindi hivyo kuwa ni Uhondo ambacho kitafanyika siku ya jumatano, Sports headquarters siku ya Alhamisi, joto la asubuhi siku ya Ijumaa na Funga mtaa siku ya jumamosi ,ambapo pia utapigwa muziki wenye ladha ya singeli kwa lengo la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki huo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano vodacom Nandi Mwiyombella alisema wanafurahi kuidhamini Efm kwa sababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon."Burudani ndio sehemu ya maisha ya kila mtu na lengo ni kuhakikisha kwamba wateja wetu anapata burudani ya muziki kupitia Efm,"amesema Nandi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...