Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi yake kuhusu utaratibu wa kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kuhusu utaratibu wa kuhamia Dodoma kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2016
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika Mkutano wa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Agosti 17, 2016 kuhusu Utaratibu wa kuhamia Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizoko chini ya Ofisi yake baada ya kuzungumza na watumishi wa Ofisi yake kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam, Agosti 17, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama , Wapili kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya kuzungumza nao kwenye ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam Agosti 17, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera, Bunge, Kazi, Vijana Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, Wapili kulia kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Abdallah Possi.
(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...