Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyuga (katikati) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA), Bw.Frank Kanyusi (kulia) na washiriki wengine wakisikiliza mada ya Naibu Msajili – Sheria za Biashara(BRELA) Bw. Andrew Mkapa katika semina elekezi kwa wafanyabiashara mkoani humo juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara na majukumu ya BRELA. Pia kuna usajili majina ya biashara na makampuni wa papo kwa papo kwa muda wa wiki nzima.

Mkuu wa mkoa wa Geita Meja general mstaafu Ezekiel Kyuga amewashauri Wafanyabiashara katika Mkoa wa Geita kurasimisha biashara zao kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) zao ili zitambulike kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa semina elekezi juu ya majukumu ya BRELA na umuhimu wa urasimishaji wa biashara na fursa zake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyuga, amewaeleza wafanyabiashara kuwa  kurasimisha biashara kuna faida zake. 

Amezitaja faida hizo kuwa ni biashara au kampuni kutambulika, kulindwa na kusaidiwa kwa mujibu wa sheria, kulipa kodi ili kujenga uchumi wa taifa na kuboresha maisha ya wananchi, kuondoa dhana duni  ya kufanya shughuli kwa mazoea na  kutengeneza mazingira bora ya biashara nchini kwa faida ya kila mwananchi na hasa wafanyabiashara wenyewe.

Amesema kwamba sekta ya biashara ina nafasi kubwa katika utekelezaji wa  hazma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati  ifikapo 2025.“Ili kutengeneza mazingira bora ya biashara nchini  ni muhimu  kurasimisha kila biashara ili zitambulike kwa mujibu wa sheria,” alisema Bw.Kyuga

Mkuu wa Mkoa alishauri wafanyabiashara watumie fursa ya kuwepo kwa maofisa wa Brela mkoani warasimishe biashara zao. “ Brela wametuthamini. Wametufuata huku tuliko. Tutumie nafasi hii vizuri ili turasimishe shughuli zetu kwa urahisi.”
  
Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw.Frank Kanyusi, amesema  kwamba Brela imefanya maboresho mengi katika huduma za usajili na kuongeza kwamba lengo la kuwepo mkoani  kwa juma moja ni kutoa elimu ya urasimishaji biashara, kuwapa fursa wananchi kusajili majina ya biashara na makampuni na kuwaomba  wakazi wa Geita kurasimisha biashara zao katika kipindi hiki.

Bw Kanyusi ameeleza kuwa  usajili wa majina ya biashara unafanywa kwenye mtandao hivyo mfanyabiashara hana sababu ya kusafiri hadi Dar es salaam na kuongeza  kuwa Breka inapigana ili huduma zote za usajili wa majina ya biashara, makampuni, alama za biashara zipatikane kwa njia ya mtandao ifikapo Machi, 2017.

 Ameeleza kuwa biashara inakuwa rasmi inapokuwa na cheti cha Brela, nakala ya namba ya mlipa kodi(TIN) na Leseni ya Biashara na kueleza huu  ndiyo  msingi wa elimu inayotolewa na wakala juu ya  urasimishaji biashara.

Katibu wa TCCIA mkoa wa Geita, Bi.Mariam Mkaka, ameishukuru Brela kuwa uamuzi wake wa kufungua ofisi za kanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara kurasimisha biashara zao.

BRELA inaendelea kutoa semina elekezi na usajili wa majina ya biashara na makampuni kwa Kanda ya Ziwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kutoa elimu kwa kanda zote nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...