Na Faustine Ruta, Bukoba
Mchungaji King James wa Kanisa la Pentekoste Assemblies of God (P.A.G) kutoka Maeneo ya Kahororo Kyamaizi Bukoba, King James ambaye pia ni  mmoja wa wadau wa maendeleo Manispaa ya Bukoba Leo jumatano septemba 14, 2016 jioni amewatembelea Waathiriwa wa Tetemeko na kuwafariji Wananchi. Ni baada ya maafa kutokea katika janga la tetemeko la ardhi, lililotokea jummosi iliyopita mkoani hapa Kagera, ambapo imeripotiwa idadi ya vifo kuongezeka na kufikia watu 17, huku wengine 253 wakijeruhiwa na kusababisha simanzi na masikitiko kwa familia nyingi. Katika tukio hilo, pia nyumba 840 za makazi zimeanguka, nyumba 1,264 zimepata nyufa kubwa na majengo 44 ya taasisi mbalimbali zikiwemo shule kuanguka. King James ametembele sehemu tofauti tofauti kama Kata ya Hamugembe, Kashai, Rwamishenye na kutoa Misaada ya dharura kama Mahema, mchele, Sukari na Pesa taslimu na kuwaombea pia. Mchungaji James pia kesho ataendelea kutoa Misaada kwa Wahanga wa Tetemeko la Ardhi la nguvu ya 5.7 katika vipimo vya Richter lilitokea eneo la Bukoba, kaskazini magharibi mwa Tanzania ambalo limeathiri sehemu kubwa ya Wanakagera kuanzia kwenye Makazi yao na wengine kukosa makazi na mpaka sasa kulala nje kutokana na nyumba zao kubomolewa.Takribani shilingi bilioni 1.4 zimepatikana mpaka sasa katika harambee iliyoongozwa na serikali ili kusaidia athari za tetemeko la ardhi hapa mkoani Kagera. 

Hamugembe Omukishenye ni sehemu kubwa iliyoathiriwa na tetemeko la Ardhi na Nyumba Nyingi kuanguka na nyingi kubomoka huku ikiwa imepoteza zaidi ya Wakazi 6. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...