Kamati ya Mpito ya Jumuiya ya
Watanzania/Wana-Diaspora Uingereza,inaitikia wito wa serikali na inapenda
kuwajulisha kuwa inaendelea na juhudi za kuwashirikisha Watanzania na marafiki
wa Watanzania duniani kote katika kuchangia maafa yaliyowapata ndugu zetu wa
mkoa wa Kagera na maeneo jirani yaliyokumbwa na maafa .
Taarifa kutoka vyombo
vya habari zinaonesha kuwa mpaka sasa ndugu zetu 20 wamepoteza maisha, na
wengine wengi wanahitaji huduma mbali
mbali za kiafya na kijamii, hususa ni matibabu na makazi ya kudumu.
Tumependekeza utaratibu wa kuchangia kwa njia
ya mtandao ili kurahisisha uchangiaji na kuweka uwazi katika kufuatilia
maendeleo ya michango. Tunawaomba Watanzania wote na marafiki wa Watanzania
walioguswa na maafa haya, tuchangie kwa hali na mali kupitia kwenye tovuti hii
hapa chini na michango hii itawakilishwa moja kwa moja kwa kamati ya maafa
ofisi ya waziri mkuu mara zoezi litakapokamilika.
Njia hii itarahisisha
kupunguza gharama za “international transaction
money transfer fee” hasa kwa wanadiaspora na marafiki zao wanaotaka
kuchangia kwa kiasi kidogo kidogo kama £10, $10, or
10 euro nk. Idadi ya watu wa namna hii ni kubwa sana, ambayo itasaidia
kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha zoezi hili.
Kamati ya mpito inawajulisha Watanzania wote
waishio Uingereza kuwa hivi karibuni ilialikwa Ubalozini na kukutana na Balozi
wetu Dr Asha-Rose Mtengeti Migiro. Maongezi yalikuwa mazuri na bado
yanaendelea.
Kwa sasa tunawaomba tuungane kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu, wale
wote waliopoteza maisha yao na pia, kuwaombea majeruhi ili wapone haraka.
Tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kuwachangia ndugu zetu katika kipindi
hiki kigumu.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu
atuzidishie moyo
wa upendo ili “Tuwapende Majirani zetu kama Tunavyojipenda”.
Ili kuchangia bonyeza link hapa
chini
Mungu Ibariki Tanzania.
Eng. Dr Julius Hingira
Abraham Sangiwa
Mwenyekiti – Kamati ya Mpito.
Katibu Mkuu – Kamati ya Mpito
TZUK DIASPORA / TANZUK
TZUK DIASPORA / TANZUK
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...