Waziri nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, uratibu, bunge, vijana na watu wenye ulemavu) Mhe  Jenister Mhagama ametoa siku saba kwa taasisi za serikali, wizara,makampuni na watu binafsi kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Vilevile Waziri Mhagama imeiagiza Bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii kuhakikisha wanawasukuma wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.

Waziri Mhagama alitoa tamko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni huku akitumia fursa hiyo kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara yake, Bw Erick Shitindi  kuhakikisha uongozi wa mifuko hiyo unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote walioshindwa kulipa madeni yao.

“Ninafahamu fika kuna mikataba ambayo ilisainiwa na pande zote mbili kabla ya kutolewa kwa hiyo mikopo na makubaliano mengine hivyo naomba basi mikataba hiyo itumike kufanikisha agizo hili,’’ alisema.

Pia alimuagiza  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe kuhakikisha kwamba anampatia ripoti muafaka  ya utekezaji wa agizo hilo.
"Kwa niaba ya serikali, ninataka kuona kwamba wadaiwa wote wa mifuko hii bila kujali nafasi zao kiuchumi au kisiasa wanalipa madeni wanayodaiwa…hii lazima ijumuishe makampuni, wawekezaji na taasisi za serikali,’’ alisema.
Awali, Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya mfuko wake kufanikisha utekelezeaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na zile binafsi wakiwemo pia wale walionunua nyumba za shirikal hilo.
Kwa mujibu wa Prof. Kahyarara, shirika hilo bado linadai takribani sh bilioni 20 kutoka kwa wa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za kimarekani milioni 1.2.Kiasi kingine cha bilioni 86 kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa waajiri walioshindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao.
Madeni mengine ni pamoja na deni la sh milioni 42 na Dola za kimarekani milioni 35.9 ambazo zilitolewa  kama mikopo kwa sekta binafsi mbalimbali huku mkopo mwingine  wa sh bilioni 38 ulitolewa kupitia SACCOS na bado hazijarejeshwa.
“Hata hivyo tumeanza kuchukua hatua mahususi kwa kulingana na matakwa ya sheria kuhakikisha kwamba madeni yote yanalipwa,’’ alibainisha Prof Kahyarara.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu huo kufuatia mikopo hiyo shirika litachukua hatua dhidi  wadeni wake hatua iliyosababisha baadhi ya wadaiwa hao kwenda mahakamani kupinga huku uamuzi wa mahakama kuhusu suala hilo ulitarajiwa kutolewa leo (Jumatatu).
Akiwa kwenye miradi ya shirika hilo Waziri Mhagama alionyesha kuridhishwa na miradi hiyo iliyoanza mwaka 2014 na inatarajiwa kukamilika mwisho mwa mwaka 2016 ukihusisha ujenzo wa nyumba 439 ambazo zitauzwa kwa bei nafuu zikiwemo zile ambazo zitapangishwa. 
 Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu   Mhe. Jenister Mhagama akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe.
 Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama akiwa ameambatana na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe. (kushoto) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu  Mhe. Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia). 
 Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara (kulia) akizungumza mbele ya Waziri nchi ofisi ya waziri mkuu sera, uratibu, bunge ,vijana na watu wenye ulemavu Mhe.  Jenister Mhagama wakati waziri huyo alipotembelea miradi ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mwishoni mwa wiki. Wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF Prof Samwel Wangwe (kushoto).




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...