Shirika
la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF) limewasilisha
mapendekezo kwa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria likitaka kufutwa kwa
sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo
zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini .
Akizungumza
katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga amesema
mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi
kikubwa zimekuwa zikiwakanadamiza wanawake na kuwanyima haki ya
kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na
waume zao.
Amesema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba
Serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini
itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika
urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanaume ikiwa ni pamoja na watoto wa
kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa
kiume amefariki.
“Tulipoonana na Mhe Waziri Dkt Mwakyembe
alituagiza kama tunataka kuwasaidia wanawake nchini basi tuwasilishe
wizarani mapendekezo yetu juu ya nini kifanyike, sasa leo tumekuja hapa
kutekeleza agizo la Mhe Waziri, tunampatia Katibu Mkuu mapendekezo
husika, ambayo kwa asilimia kubwa yanapendekeza kufutwa kwa sheria zote
za kimila ambazo zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike na kutungwa
kwa Sheria moja itakayoshughulikia masuala yote ya mirathi nchini na
tuna imani kuwa yatafanyiwa kazi na kufanikisha azma ya WILDAF ya
kuwasaidia wanawake nchini, alisema Mwenyekiti wa WILDAF Bi. Judith
Odunga
Akipokea mapendekezo hayo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam
amewapongeza na kuwashukuru WILDAF kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya
ili kuwasaidia wanawake na Serikali kwa ujumla wake kwani kitendo
hicho kitasaidia sheria husika kufanyiwa marekebisho yatakayostahili
ili ziendane na wakati, zikidhi mahitaji na kutafsiriwa katika lugha
ambayo wananchi wengi ambao ndio walengwa wazielewe sheria hizo
Amesema
sasa Serikali imedhamiria kuhakikisha kuwa sheria zote nchini
zinatafsiriwa na zile zinazotungwa zitakuwa kwa Kiswahili na Kingereza,
uamuazi ambao utawawezesha watanzania wengi kuzielewa sheria hizo.
Prof
Mchome alaiwashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaadi kuwa
wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yaoi ili
kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia
wananchi wengi na kuwataka wadau wengine kuja wizarani kuzungumza pale
watakapoona kuna haja ya kufanya hivyo kwani wizara ipo tayari
kuwasilikiza na kuyafanyia kazi mapendekezo yao.
Mkurugenzi wa WILDAF Bi. Judith Odunga akipeana mkono na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijni Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo hayo yanayotaka kufutwa kwa sheria za kimila nchini ambazo zinadaiwa kuwakandamiza wanawake kwa kuwanyima haki sawa ya kumiliki mali pindi wanapofiwa na waume au wazazi wao anaeshuhudia kushoto ni Bibi Thabita Siwale Mwenyekiti wa Kikosi cha kupambana na haki za mirathi Tanzania- KIKUHAMI.
Wajumbe mbalimbali wa WILDAF walioambatana na Mwenyekiti kushuhudia uwasilishaji wa mapendekezo yao wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome Ofisini kwa jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...