GAVANA WA BENKI KUU YA TANZANIA PROFESA BENNO NDULLU

Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, alipoingia madarakani mwezi Novemba 2015 aliendeleza jitihada za kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuweka mkazo na kutoa maagizo kwenye maeneo kadhaa.
Maeneo hayo ni pamoja na; kuongeza nguvu kwenye ukusanyaji wa kodi, kupiga vita rushwa, kuweka msisitizo mkubwa wa nidhamu ya matumizi ya fedha za umma, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza matumizi katika sekta za vipaumbele vya maendeleo. 
Aidha, kuzitaka Wizara, Wakala na Taasisi za Umma kuweka fedha zao Benki Kuu na kuhimiza kila mtu afanye kazi na kula kwa jasho lake ili kutekeleza falsafa ya ‘Hapa kazi tu’. 




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...