HATIMAYE waimbaji wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi
sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali leo Oktoba 22
ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala. Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya
jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa
masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia
wa taarab.
Bendi
mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic
zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla. Waimbaji hao wawili kwa
pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa baada ya majigambo mengi kutoka
kila pande, leo mzizi wa fitna utakatwa ndani ya Dar Live.
Leyla
Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki
mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe
Isha hawezi kuyagoka. Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa
na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange
huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...