Basi
lenye namba za usajili T990 AQF la kampuni ya Safari Njema liililokuwa
likitokea Dodoma kuja jijini Dar, limeteketea kwa Moto maeneo ya Kimara
Stop Over-Suka,mara baada ya kugongana na Lori lililokuwa limebeba shehena ya mifuko ya Cement (namba zake
za usajili hazikujulikana mara moja),jioni ya leo,Inaelezwa kuwa mali zote zilikowemo katika
basi vimeteketea kabisa kwa moto,hali ya abiria waliokuwemo ndani ya
basi hilo tutawaleta taarifa kamili itakayotolewa na Jeshi la Polisi.
UPDATES
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
UPDATES
Jeshi la Polisi limeeleza kuwa mtu mmoja amefariki Dunia katika ajali hiyo na wengine 16 wamejeruhiwa na baadae kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu.
Pichani
Lori kama lionekavyo likiwa nyuma ya basi baada ya kugongana
kusababisha mlipuko mkubwa wa moto na kupelekea magari yote mawili
kuwaka moto .
Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.
Baadhi ya Wakazi wa eneo la Kimara Stop Over na Kimara Suka wakielekea kushuhudia eneo la ajali kati ya basi la Safari Njema na Lori lililokuwa limebeba shehena kubwa ya mifuko ya Cement.
Baadhi ya mashuhuda wakishuhudia tukio hilo lilivyokuwa
Gari la zima moto likiwa eneo la tukio kuuzima moto huo.
Baadhi
ya Vijana wasio waaminifu walivamia eneo hilo la ajali na kuanza
kuondoka na mifuko ya Cement iliyokuwa imebebwa na Lori hilo.
hata utu umekwisha sasa baada ya kutoa msaada unaiba aibu kweli kweli
ReplyDeleteDuuuuh
ReplyDeletePOleni sana
ReplyDelete