NA MAGRETH MAGOSSO,KIBONDO.

SHIRIKISHO la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kwa kushirikiana na Kampuni ya kutengeneza magari ya Chivrolet ya Marekani imewakabidhi mipira 60 kwa ajili ya Soka la Watoto walio chini ya miaka 12 kwa shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR la kuhudumia wakimbizi katika Kambi ya Nduta iliyopo wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenye kambi ya Mtendeli zote za Mkoa wa Kigoma .

Akithibitisha hilo juzi Mkuu wa UNHCR Kibondo Dost Yousafzai alisema wamepokea mipira hiyo kwa nia ya kuwaunganisha na kuthaminiana baina ya watanzania na warundi katika tasnia ya michezo hususani katika soka la mpira wa miguu kwa watoto waishio kambini kwa kuwa wafrika wote ni ndugu .

Alisema pamoja na UEFA na kampuni hiyo kutoa kwa ajili ya kambi hizo,shirika la UNHCR wametoa mipira 20 kwa ajili ya vijiji vinavyoishi karibu na kambi ya nduta ya kibondo na mipira 20 kwa vijiji vinavyoishi jirani na kambi ya mtendeli,ili waratibu wa chama cha mpira wilayani humo wagawe kwa timu hai ili kuimarisha michezo baina ya raia na wakimbizi.

Akipokea mipira hiyo kwa niaba ya wanakijiji Katibu wa Chama cha mpira Kibondo James Evalist alisema kwa leo anachukua mipira 10 tu,na mipira miwili aliikabidhi kwa timu ya Birutana ambayo inashiriki mashindano ya mechi za ujirani mwema baina ya Burundi na Tanzania huku mipira 10 ikisalia kwa mkuu wa UNHRC.

’ mipira ya watoto haihimili vishindo kwa timu za wakubwa, siikatai na nawashirikisha wanamichezo wa kibondo lakini kama mmeamua kutusidia mlete mipira inayokidhi mahitaji ya timu za wakubwa lakini tunaomba mturekebishie uwanja wa Mpira kwa kuwa uwanja uliopo ni una kokoto tupu, alisema James. 

Naye Kaimu Mkuu wa makazi Kambi ya Nduta Jesca Ntaita alitoa mwito kwa Watanzania na Warundi wanaoishi katika makambi ya wakimbi kufuata taratibu za nchi kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania huingia makambini kwa vibali vya warundi na warundi vivyo hivyo.

Na Mtendaji wa kijiji cha Biturana Henry Thomas alisihi shirika la UNHCR kuwa waendeleze mashindano ya ujirani mwema baina ya raia wa pande zote mbili waishio katika kambi hizo,kuwa yasiishie kambini bali yaongeze wigo wa mashindano hayo.

Aidha kudhihirisha kuwa wanaweza kusakata kabumbu timu ya kambi ya mtendeli iliwabugiza goli 4-0 dhidi ya Timu ya kijiji cha Kasanda huku timu ya kambi ya nduta iliwafunga bao 2 Timu ya Kijiji cha Biturana ya wilayani.mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...