SIMU.TV: Bunge la nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki linaendela Visiwani Zanzibar ambapo limepokea hoja binafsi kutoka kwa mbunge wa Tanzania kuhusu kutunga sheria ya kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi. https://youtu.be/QMpPY7OZYr0

SIMU.TV: Wananchi katika kata tatu wilayani Hanang wapo hatarini kupatwa na magonjwa ya kansa kutokana na kuchafuliwa kwa vyanzo vya maji wanavyotumia.https://youtu.be/v7XiAirCGj8

SIMU.TV: Serikali imesema licha ya uchumi wa nchi kukua bado theluthi ya watanzania ni masikini na kiwango cha umaskini kwa watanzania kinapungua kwa kasi ndogo sana.https://youtu.be/YQ4OIwvhZz0

SIMU.TV: Kaya nne katika kijiji cha Tindigan wilayani Siha mkoani Kilimanjaro zimebomolewa nyumba zao baada ya kujenga eneo lenye mgogoro. https://youtu.be/UMytAvpNqyQ

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam amewataka wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam kutumia fursa ya ujio wa Mfalme wa Morocco kujenga fursa za kiuchumi.https://youtu.be/R8zbU6daA4s

SIMU.TV: Waziri wa fedha na mipango ameyataka mabenki na taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali. https://youtu.be/4alMkKCTd2E

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabiashara wadogo wamelalamikia kuendelea kutozwa ushuru licha ya serikali kupiga marufuku ushuru kwa wafanyabiashara wadogo.https://youtu.be/4KCVV8nLQUY

SIMU.TV: Kampuni ya Zuku TV inayomilikiwa na Wananchi Group imefanikiwa kuboresha huduma zake na kuongeza ajira kwa mwaka 2016. https://youtu.be/2nbsT0L-bVw

SIMU.TV: Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia mwenyekiti wao Yusuph Manji umewataka wananchama kuhudhuria mkutano wao wa dharura jumapili ili kila mmoja aweze kutoa maoni yake badala ya kuongea kwenye vyombo vya habari. https://youtu.be/uzfdFaz1TOM

SIMU.TV: Timu ya Kagera Sugar Kesho inakabiliwa na kibarua kigumu katika uwanja wake wa Kaitaba kwenye mchezo dhidi ya mabingwa watetezi timu ya Yanga.https://youtu.be/IMVEsdEk5-w

SIMU.TV: Zaidi ya wachezaji mia moja kutoka maeneo mbalimbali nchini wamejitokeza kushiriki katika mashindano ya wazi ya Gofu ya PWC katika viwanja vya Lugalo.https://youtu.be/lohkcvdeszA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...