NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
SHIRIKA la umeme nchini (TANESCO), limekamilisha
ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji
umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) , kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya
Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda
kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha
ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.
Akizungumzia maendeleo ya utekelezaji
wa mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa
Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa
njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa
kilomita 4.3 wa msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City
Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi
alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi
(Underground Transmision Lines), kwa
msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika
na ule wa kutoka shule ya sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre
pia umekamilika.
Kaimu Meneja Mradi wa uboreshaji wa huduma za umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), kwenye shule ya sekondaru ya wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Hendry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuja shule ya sekondari ya wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya jiji
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...