Na Lulu Mussa- Kigoma 

Shirika lisilo la Kiserikali la Jane Goodall linalojishughulisha na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori wengine limepongezwa kwa jitihada zake za kutunza mazingira na kusaidia jamii kuhifadhi mfumo wa ikolojia ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. 

Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba mara baada ya kutembele Ofisi zao Mkoani Kigoma. Waziri Makamba amesema kuwa Shirikal hilo la Jane Goodall limekuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi ambayo inagusa jamii moja kwa moja. 

Akitoa maelezo ya shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo kwasasa, Naibu Mkurugenzi wa Bi. Mary Mavanza amesema kuwa wanatekeleza miradi mitatu ikiwa ni pamoja na Mradi wa utafiti wa sokwe na wanyamapori, Mradi wa Mizizi na chipukizi ambao unatekelezwa nchi nzima katika shule zote na mradi wa uhifadhi unatekelezwa katika Halmashauri za Wilaya za Mpanda, Nsimbo kwa Mkoa wa Katavi na Uvinza kwa Mkoa wa Kigoma. 

Aidha, Shirika hili pia limefanikiwa kuhamasisha wanajamii 42 kufanya shughuli za kukuza kipato ambazo ni rafiki kwa mazingira kupitia ufugaji nyuki na huduma za ki ikolojia. Pamoja na mafanikio hayo shirikali hili limewasilisha hoja ya kwa Waziri Makamba kusaidia kukamilika kwa Mchakato wa kupandisha hadhi ya ardhi jumla kuwa misitu ya Hifadhi ya Wilaya ili kudhibiti idadi kubwa ya sokwe waliobaki Tanzania ambao kwa sasa hawana ulinzi thabiti. 

Taasisi ya Jane Goodall liliasisiwa miaka 56 iliyopita na mtafifiti Dr. Jane Goodall kwa lengo la kufanya shughuli za kitafiti, kurejesha uoto wa asili uliopotea na kuhakikisha wanajamii wanaboresha uchumi wao kwa kutumia maliasili zinazowazunguka. Waziri Makamba pia ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe kwa lengo la kufuatilia changamoto za kimazingira Hifadhini hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akiwa katika boti Maalumu kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Gombe Bw. Donatus Bayona (kulia) na Bi.Happy Kiyemi Mkuu wa Idara ya Utalii wakimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kutembelea Hifadhi ya Gombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Shirika lilisilo la Kiserikali la Jane Goodall, mara baada ya Mhe. Waziri Makamba kutembelea Ofisi zao Kigoma Mjini. Wa kwanza kulia ni Bi. Mary Mavanza Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa kuhifadhi mfumo wa Ikolojia Ukanda wa Magharibi mwa Tanzania. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Bw. Samson Anga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...