Na. Immaculate Makilika - MAELEZO
BARAZA la Madiwani ya Halmashauri ya Mji wa Bunda limemfukuza kazi Bw. Eliud Haonga aliyekuwa mtumishi wa Idara ya Ardhi na Mipango na Mthamini daraja la pili mapema wiki hii, baada ya kughushi nyaraka ili kujipatia fedha za malipo ya pango.
Bw. Haonga alipokea fedha za malipo ya pango kiasi cha shilingi milioni saba kutoka kiwanda cha OLAM Tanzania mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mkoa wa Mara, Bi. Janeth Mayanja alisema kuwa Bw. Haonga amekiuka Sheria za Utumishi wa Umma, kanuni ya 42 na uamuzi uliotolewa na baraza la madiwani ni sahihi.
Bi. Janeth alisema “Bw. Eliud Haonga alihifadhi shilingi milioni mbili tu katika akaunti ya Halmashauri ya Mji wa Bunda na kutumia shilingi milioni tano kwa matumizi yake binafsi”.“Maamuzi haya yamechukuliwa baada ya Kamati ya Uchunguzi kumaliza kazi yake kwa mujibu wa Sheria, kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma.” alisema Bi. Mayanja.
Aidha, Bi. Mayanja amewaasa watumishi wa Halmashauri Bunda kujiepusha na vitendo vinavyoashiria wizi na ubadhirifu, na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maadili ya utumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoa wa Mara Bi. Janeth
Mayanja akiwa Ofisini kwake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...