Bado dunia na ulimwengu wa soka kwa sasa unaomboleza msiba wa msafara wa timu ya Chapocoense ya Brazil uliyopata ajali wakati wakielekea kutua uwanja wa ndege wa Medellin Colombia. 

 Ajali hiyo ya ndege imehusisha watu 81 kati ya hao 76 wamepoteza maisha huku 72 kati ya hao walikuwa ni sehemu ya msafara wa timu hiyo na wachezaji wakielekea kucheza mchezo wao wa fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Amerika kusini dhidi ya Atletico Nacional ya Colombia. 
 Cristiano Ronaldo ni mmoja kati ya mastaa wa soka walioguswa kwa kiasi kikubwa na msiba huu, Ronaldo ameamua kuchangia euro milioni 3 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.6 kwa timu ya Chipacoense na familia za wachezaji wa timu hiyo waliyo poteza maisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...