Na. Lilian Lundo – MAELEZO - Mara

Halmashauri tatu za Mkoa wa Mara zimevuka Lengo la Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN) la asilimia 80 katika matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2016.

Hayo yamesemwa leo, Wilayani Tarime na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mara Mwalimu  Hamis Lissu alipokuwa akifungua semina ya Mawasiliano na kushirikishana jitihada zenye mafanikio kwenye Elimu kwa maafisa wa Elimu wa Mkoa wa huo.

“Halmashauri za Tarime Mji, Tarime Manispaa na Musoma Manispaa ni halmashauri ambazo zimevuka lengo la BRN katika Mkoa wa Mara, Halmashauri hizo kila moja zimepata wastani wa asilimia 82 katika matokeo ya darasa la Saba ya mwaka, 2016,” alifafanua Lissu.

Aliendelea kwa kusema kuwa, ufaulu wa darasa la saba katika Mkoa wa Mara umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka 2014, ambapo kwa mwaka 2014 Mkoa wa Mara ulikuwa Mkoa wa 25 kati ya Mikoa 25, mwaka 2015 Mkoa ulishika nafasi ya 17 kati ya Mikoa 25 na mwaka huu 2016 umeshika nafasi ya 13 kati ya Mikoa 26.

Lissu amesema kuwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mara zimeongeza ufaulu katika matokeo ya mwaka huu ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015 na 2014.Vile vile amesema kuwa ongezeko hilo la ufaulu limefanikishwa kwa kiwango kikubwa na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality Improvement Programme -Tanzania) EQUIP-T  unaosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza.

Mpango huo umekuwa ukitoa mafunzo ya kuboresha utendaji wa walimu darasani pamoja na kutoa pikipiki kwa waratibu elimu kata wote ambao ndio wafuatiliaji wakubwa wa ufundishaji wa walimu na maendeleo ya taaluma ya mwanafunzi katika ngazi ya kata.


Aidha Lissu amesema kuwa kuna asilimia kubwa ya Mkoa huo kushika nafasi ya kumi bora kitaifa katika matokeo ya mwaka 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...