Na George Binagi-GB Pazzo

Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Dkt.Leonald Subi, amewahimiza wananchi kuwa na desturi ya kupima afya zao mara kwa mara hususani kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili kuepukana na madhara yake ikiwemo vifo vinavyofikia asilimia 27 nchini.

Dkt Subi aliyasema hao wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya bure ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi mkoani Mwanza, inayofanyika kwa siku mbili kuanzia jana katika Uwanja wa Furahisha, Vituo vya afya Igoma, Karumbe na Makongoro.

Aidha Dkt.Subi aliwahimiza wanajamii kubadili mfumo wa maisha kwa kuzingatia kanuni za afya ili kuepukana na madhara yatokanayo na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ni pamona na kansa, presha pamoja na kisukari.

“Magonjwa haya yanatokana na namna ya maisha tunavyoishi ikiwemo kutokufanya mazoezi, ulaji wa chakula usiozingazi kanuni, ulevi, uvutaji wa sigara, kuwa na wapenzi wengi na kutokuzingatia kanuni za afya kwa ujumla”. Alisema Dkt.Subi.

Kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi inaratibiwa na Chama cha Madaktari Wanawake nchini MEWATA katika mikoa ya Mwanza, Iringa na Mbeya kwa lengo la kuhamasisha wananchi kupata huduma mapema kwani magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo saratani hutibika ikiwa mgonjwa ataanza matibabu mapema.
Dkt.Leonald Subi


Tazama HAPA Picha za Uzinduzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...