Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MAKAMU Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga amemtambulisha rasmi kocha mkuu wa timu hiyo Mzambia George Lwandamina, aliyechukua nafasi ya Mholanzi  Hans Van De Pluijm aliyevikwa viatu vya Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.

Lwandamina anachukua mikoba ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyebadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa ufundi ili kumsaidia Mzambia huyo katika masuala mbali mbali ya maendeleo ya klabu hiyo, na moja kwa moja Mzambia huyo huku mzambia huyo akafunguka juu ya kikosi atakachoingia nacho vitani.

Sanga ameweka wazi kuwa ujio wa kocha huyo sasa ni rasmi na wamempa kandarasi ya miaka miwili,lengo kubwa ikiwa ni kuongeza nguvu kwenye kikosi cha wanajangwani hao katika kutetea Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom na michuano ya kimataifa. 

"Uongozi wa Yanga leo hii unayo furaha kuwatambulisha kocha mkuu George Lwandamina na Mkurugenzi wa ufundi Hans Van De Pluijm, tunaamini kwa pamoja wataweza kuipa mafanikio zaidi timu yetu kutoka hapa ilipo na kusonga mbele zaidi" amesema Sanga.

Baada ya utambulisho huo, Kocha mkuu Lwandamina akafunguka na kusema kuwa ni changamoto mpya kwake kwani anajua Yanga ni klabu kubwa na amepewa nafasi hiyo na kwa kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla na wachezaji kwa pamoja atahakikisha anatumia kila kinachowezekana kuhakikisha Yanga inafanya vizuri kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi klabu Bingwa Afrika. 

Akaeleza kuwa kuna habari zinazoenea kuwa anakuja na wachezaji wapya kutoka Zesco, akasisitiza zaidi kuwa "Nasikia tetesi kuhusu wachezaji wapya kutoka Zesco kusajiliwa Yanga mimi kama kocha mkuu sijui chochote labda michakato hiyo inafanyika bila mimi kushirikishwa kikosi kilichopo ndicho nitaendelea nacho". 

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Pluijm akawa na yake ya kusema na kueleza kuwa hana shida na kubadilishiwa majukumu na zaidi ataendelea kushirikiana na benchi la ufundi kwa ujumla katika kuhakikisha wanaendelea kutetea ubingwa wao na kufanya vizuri kwenye kombe la Klabu Bingwa Afrika.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akimkabidhi jezi ya timu hiyo Kocha Mkuu George Lwandamina leo Jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu George Lwandamina akisalimiana Mkurugenzi wa benchi la Ufundi Hans Van De Pluijm ambaye awali alikuwa ndiye kocha Mkuu.
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Clement Sanga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa kocha mkuu  Mzambia George Lwandamina (kulia) pamoja na nafasi ya Mholanzi Hans Van De Pluijm aliyechukua nafasi ya mkurugenzi wa ufundi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...