Na Tiganya Vincent-MAELEZO- Dar es salaam.

Novemba 5, mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alioapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka mmoja cha utawala wa Rais Magufuli nchini, Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa upande wake umesaidia Watanzania wanaopata huduma za Jamii kupitia PSPF kuongezeka kutoka 394,494 hadi kufikia 444,679 ikiwa ni sehemu ya utekeleza wa agizo lake. 

Hatua hii ya PSPF imelenga kutekeza agizo na kutimiza ahadi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyokuwa akitoa ya kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanufaika na huduma za Hifadhi za Jamii ikiwemo huduma za Bima za afya wakati wa kampeni na baada ya kuingia madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja kwa upande wa Mfuko wa PSPF iliyotolewa na Costantina Martin kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSPF ,idadi hiyo hii inajumuisha Watanzania walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi nchini. 

Kundi hili kubwa lilikuwa limesaulika kujumuishwa katika hifadhi ya jamii , lakini baada ya Mhe. Rais Magufuli kulizungumzia katika kampeni zake hivi sasa mwamko wa kujiunga na hifadhi ya jamii umeongezeka na PSPF imeanza kulitekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha wananchi waliopo katika sekta isiyo rasmi na sekta rasmi kuchangia na kujiunga katika Bima ya Afya.
 
Katika kuhakikisha kuwa azma hiyo inatimizwa tayari PSPF imeingia makubaliano na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) kwa lengo la kufikisha huduma za afya kwa watanzania wengi ambao wapo katika sekta isyo rasmi na hivyo kujenga jamii yenye afya bora inayochangia katika ujenzi wa nchi.

Chini ya makubaliano yanawasaidia wanachama wa PSPF walio katika Mpango wa Uchangiaji wa Hiari kuweza kupata ya tiba kupitia NHIF kwa gharama ya shilingi 76,800/- kwa mwaka katika hospitali mbalimbali ziliingia makubaliano na Mfuko huo wa Bima ya Afya.Mpango huo wa PSPF unaounga mkono juhudi za Rais Magufuli za kutaka kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanapata huduma na matibabu nchi nzima kwenye vituo vyote vilivyosajiliwa na NHIF kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa kwa gharama nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...