Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii

Serikali imeamua kuandaa shindano la Kitaifa la kutafuta Mbadala wa Mkaa kwa lengo la kuwatambua, kuwatuza, kuwawezesha na kuwaendeleza wabunifu na wajasiriamali wanaojihusisha na mbinu na jitihada za uzalishaji, usambazaji na matumizi ya nishati endelevu za kupikia.

Hayo yamezungumzwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh.January Makamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi ya makamu wa Rais iliyopo jijini dar es Salaam, amesema dhumuni la kuanzisha shindano hilo ni kuwaleta pamoja wadau na wabunufu wanaojishughulisha na harakati za kutafuta na kutumia Nishati Mbadala wa mkaa.

"katika shindano hili tunatarajia kuinua uelewa juu ya ukataji miti na umaskini wa nishati,kuhamasisha ujasiriamali, kubaini makundi yanayojishughulisha na ubunifi pia kuonekana kwa mawazo na fikra mpya za watu wengi wanaojishughulisha na kupunguza matumizi ya mkaa."

Amesema katika shindalo hilo zitatolewa fursa mbalimbali kwa washindi ikiwapo fedha taslim kwa washindi watatu ambapo mshindi wa kwanza atapokea tuzo ya fedha Taslim ya shilingi Milioni Mia tatu (300,000,000) na mshindi wa pili atapokea shilingi Milioni Mia mbili (200,000,000) na wa tatu atapokea shilingi Milioni mia moja (100,000,000) ambazo zitatumika kwa ajili ya kukuza na kuendeleza mtaji wa mradi wake alioshinda.

Makamba amesema, mbali na fedha hizo taslim pia washindi watapatiwa mafunzo ya biashara na uwekezaji kulingana na uvumbuzi wao na watatambulishwa kwa wawekezaji na kupelekwa zilipo fursa zaidi za uwekezaji ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kupanua na kuupeleka sokoni ubunifu wao.

"Imani yangu ni kwamba shindano hili litaendana na hatua nyingine za kisera za kudhibiti ukataji wa misitu, kulinda vyanzo vya maji, kuondoa umaskini wa nishati na kuifanya bei ya mkaa itokane na thamani halisi ya miti iliyotumika kutengeneza mkaa huo."

Hata hivyo,amewaomba wadau wote, watu binafsi, Makampuni binafsi, wajasiriamali, Asasi za kiraia na kijamii, taasisi zilizokuwa za kiserikali, Tasisi za elimu ya juu na Tasisi za Utafiti kushiriki katika kuitatua changamoto hii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...