Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya MNET, Yalisa Phawe akitoa hutuba fupi katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi.
 Mkuu wa Chaneli ya Maisha  Magic Bongo, Barbara Kambogi akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya mwaka mmoja na uzinduzi rasmi wa Chaneli hiyo iliyoambatana na uzinduzi wa filamu za Harusi, Mirindimo ya Pwani, Huba na nyingine  mapema wikiendi hii.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akipeana mkono wa pongezi na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocenty Mungy (kushoto) mara baada ya kumaliza kusoma hotuba wakati wa hafla ya kusherehekea maadhimisho ya mwaka mmoja na uzinduzi rasmi wa Channel ya Maisha Magic Bongo inayopatika kupitia Dstv 160 iliyoambatana na uzinduzi wa Filamu za Harusi, Huba Mirindimo ya Pwani na n.k. Channel hii ni kwa ajili ya kuonyesha filamu na vipindi vinavyotumia rafudhi ya lugha ya Kiswahili.Katikati ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Baadhi ya wasanii wa Filamu nchini wakifuatilia maadhimisho ya mwaka mmoja wa Channel ya Maisha Magic Bongo ulionda sambamba na uzinduzi wa filamu za Harusi, Mirindimo ya Pwani, Huba na Mzooka. Kulia ni Baraka Shelukindo wa MultiChoice.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwaongoza baadhi ya viongozi wakati akizindua rasmi Chaneli ya Maisha Magic Bongo mapema wikiendi hii,Wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na wapili ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Simon Mwakifamba. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...