Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- uungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba akiongea na Wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya shindano la kutafuta mbadala wa mkaa,   lilioandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.



KUHUSU SHINDANO LA KUTAFUTA MBADALA WA MKAA

Nchi yetu iko njia panda. Tuna nchi nzuri yenye bioanuai za wanyama na mimea ambazo haziwezi kufananishwa na nchi nyingine yeyote. Takriban asilimia 40 ya eneo lote la nchi limehifadhiwa kwa ajili ya misitu na wanyamapori. Hata hivyo, uharibifu wa misitu unafanyika kwa kasi ya kutisha. Takriban ekari milioni moja za misitu zinateketezwa kwa mwaka. Karibu mabonde na mifumo yote ya mito mikuu hapa nchini inaanzia kwenye misitu ambayo sasa tunaiharibu kwa kasi ya kutisha.

 Kuna mambo kadhaa yanayochangia kasi hii kubwa ya uteketezaji wa misitu hapa nchini, ikiwemo ufyekaji wa maeneo kwa ajili ya kilimo, mifugo, uchomaji wa mkaa na biashara ya kuni. Hakuna shaka kwamba mahitaji ya mkaa na kuni yanazidi uwezo wa misitu yetu ya asili kukukidhi mahitaji hayo. Mahitaji haya yataendelea kuongezeka kwa kasi kwa miaka inayokuja kutokana na ukuaji wa miji na ongezeko la idadi ya watu, kwani inaaminika kwamba ongezeko la asilimia moja ya ukuaji wa miji linasababisha ongezeko la asilimia 14 la matumizi ya mkaa.

Ikizingatia kwamba, Tanzania ni moja ya nchi zinazoongoza duniani kwa kasi ya ukuaji wa miji, kiasi kwamba ifikapo mwaka 2027 zaidi ya nusu ya Watanzania watakuwa wanaishi mijini, mahitaji na matumizi ya mkaa yatakuwa maradufu kuliko ilivyo sasa. Hivyo, ni muhimu sana hatua za haraka ni muhimu zichukuliewe sasa ili mahitaji haya ya makubwa ya mkaa yasipelekee kuangamizwa kwa misitu yetu.

Kuwa na uzalishaji endelevu wa  mkaa, au kuifanya biashara ya mkaa isiwe na tija, au mbadala wa mkaa kuwa na faida zaidi kibiashara, ni jambo la msingi kwa usalama wa nishati kitaifa, kwa kupunguza ukataji misitu na kulinda huduma zitokanazo na mifumo-ikolojia nchini, ikiwemo ulinzi wa vyanzo vya maji, utiririkaji wa maji katika mito na hivyo upatikanaji wa maji nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...