Shirikisho la Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, limefanya semina ya utendaji kwa makatibu wake wote wa matawi katika mkoa wa Dar es Salaam, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kazi zao ili kuliimarisha Shirikisho na Chama Cha Mapinduzi.

Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda alisema, katika semina hiyo iliyofanyia Novemba 30, mwaka huu, jumla ya Makatibu 32 walihudhuria na kuondoka wakiwa wameongeza upeo wao katika kazi zao za chama.

Alisema, moja ya mambo ambayo walifundwa Makatibu hao ni namna nzuri ya kuwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata wanachama wapya miongoni mwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu, kwa kuwa tegemeo na uhai wa Shirikisho hilo ni wanafunzi wa aina hiyo.

"Unajua Shirikisho linatilia mkazo sana katika kuhakikisha Makatibu wa Matawi wanashughulika kwa juhudi kubwa kuhakikisha kila wakati tunapata wanachama wapya hasa hawa wanaokuwa wanajiunga katika vyuo katika mwaka wa kwanza kwa kuwa hawa wanakuwa bado wabichi na wenye nguvu kutumikia Shirikisho na Chama kwa jumla", alisema Zenda na kuongeza.

"Shirikisho linalipa kipaumbele suala la kuingiza wanachama kutoka wale wa mwaka wa kwanza kwa sababu kuingia kwa wanavyuo wapya vyuoni kuna kuwa na maana pia kuwa wapo wanaondoka kutokana na kuhitimu masomo yao, ambao baada ya kuhitimu wanaweze kushindwa kuendelea kuwa wanachama wazuri wa shirikisho kutokana na kubanwa na shughuli nyingine".
 Katibu Msaidizi wa CCM, Daniel Zenda akiongoza semina hiyo
🔺Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo katika Ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya Umoja wa Vijana wa CCM, jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...