Mtanzania
Felistas Joseph, amechaguliwa kuongoza Kamati ya nchi za Maziwa Makuu ya Kuzuia
Mauaji ya Kimbari (International Conference on Great Lakes Region –ICGLR).
Bibi
Felistas amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo katika uchaguzi
uliofanyika mjini Pointre Noire, nchini Congo Desemba Mosi mwaka 2016. Kamati
iliyoundwa chini ya Itifaki ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari inajumuisha wajumbe 12
kutoka nchi wanachama wa ICGLR ambapo
wajumbe hao huidhinishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR (Regional Inter-Ministerial
Council- RIMC).
Bibi
Felistas ni Mkurugenzi Msaidizi katika Idara ya Huduma za Kisheria
kwa Umma Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria na amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Kitaifa ya Tanzania ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari tangu ilipoundwa mwezi Februari
mwaka 2012.
Katika
nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanda, Bibi Felistas atasaidiwa na
Makamu Mwenyekiti kutoka nchini Burundi, Katibu kutoka DRC ambao kwa pamoja wanatarajiwa
kuthibitishwa na Baraza la Mawaziri la ICGLR katika kikao chao kitakachofanyika
wiki mbili zijazo nchini Kenya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...