Na Bashir Nkoromo.

Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, amesema, anazitambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi na kuahidi kushirikiana na wafanyakazi hao kuzipatia ufumbuzi.


Mpogolo amekutana na wafanyakazi hao ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.



"Mimi nimekuwa katika chama hiki mda mrefu sana, kwa hiyo sehemu kubwa ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi nazijua hivyo nitatumia juhudi zangu na maarifa kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuisha kabisa".



"Lakini kubwa zaidi ni mimi na ninyi wafanyakazi kushirikiana kwa pamoja katika kupambana na changamoto hizi na hatimaye tukifikishe chama kunakotarajiwa, na bila shaka mnajua lengo kuu la Chama chochote ni kuwa na nguvu na inayokipa uwezo wa kuongoza kwa kushika dola", alisema Mpogolo.



Alisema, pamoja na kuwa katika Chama kwa mda wa kutosha kujifunza ana kuelewa mengi, lakini bado atahitaji ushauri kwa baadhi ya wafanyakazi wazoevu, hivyo wafanyakazi wasisite kumpa ushauri wao pale watakapokuwa wanaona kwamba ushauri wao utasaidia kusonga mbele.



Mpogolo aliwataka wafanyakazi kuongeza bidii ya kazi kila mmoja katika nafasi yake, akisema ni lazima watambue kuwa kila mfanyakazi wa Chama katika eneo aliloko mchango wake unahitajika sana, na aelewe kuwa isingekuwepo haya ya chama kumwajiri kama hakitarajii tija kutoka kwake.



Mapema, Mpogolo aliwasili ukumbini akifuatana na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Balozi.



Luhwavi aliwaomba wafanyakazi kumpa ushirikiano Naibu Katibu Mkuu huyo mpya akimwelezea kuwa ni Kada wa Chama ambaye amefanya kazi katika idara nyingi na nyeti hivyo anayo hazina ya mambo mengi anayofahamu katika chama.

Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na wafanyakazi wa Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja. PICHA BASHIR NKOROMO
 Wafanyakazi wakiwa tayari kumsikiliza Mpogolo

 Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM, Rodrick Mpogolo akiingia ukumbini kuzungumza na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Utawala bakari Hamad na wapili ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utawala na Uendeshaji, Salum Khatib Reja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...