Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewapandisha vyeo Maafisa Wakuu wawili wa JWTZ kuwa Meja Jenerali kuanzia tarehe 03 Disemba 2016. Maafisa Wakuu hao ni;
Brigedia Jenerali George William Ingram ambaye ni Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga, na  Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo ambaye ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.
                                          Brigedia Jenerali George William Ingram
Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga
Brigedia Jenerali Michael Wambura Isamuhyo
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Adolf Mwamunyange kwa niaba ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu anawapongeza na kuwatakia kheri katika vyeo vyao vipya.

                            Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na 
Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638/0756-716085

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...