Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala watano kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Vijana walio hitimu Mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana 1,811 kutoka jiji la Mbeya na Wilaya ya Rungwe Mafunzo yaliyoratibiwa na shirika la Techoserve,

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala amewaagiza wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Mbeya kutenga maeneo kwa ajili ya wajasiriamali wakiwemo Vijana ili wafanye biashara na viwanda vidogo vidogo.

Hayo ameyasema wakati akifunga Mafunzo ya ujasiriamali kwa Vijana 1,811 kutoka jiji la Mbeya na Wilaya  ya Rungwe mafunzo yaliyoratibiwa na shirika la Techoserve

Aidha amewataka kutenga fedha kupitia mapato ya ndani na kutoa mikopo nafuu kwa Vijana na wanawake kwa kufanya hivyo itasaidia Makundi hayo kuanzisha biashara na kukuza biashara zao.

Pia amewataka Vijana kutobweteka badala yake wajishughulishe na kutumia fursa zilizopo katika jamii ili kujipatia kipato.

Amesema hakuna serikali itakayokuja na kuwafuata vijiweni ili iwapatie fedha bali itahahakikisha inatenga maeneo ya kufanyia biashara au kilimo kwa ajili ya Vijana wenye kuhitaji jufabya shughuri hizo. Pia mkuu wa Mkoa amezitaka Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya mikopo ya riba nafuu kwa vijana.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,  Mh. Amos Makala akizungumza na wahitimu wa mafunzo ya Ujasiliamali yaliyofanyika katika ukumbi wa Tughimbe Mafiati Jijini Mbeya.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya ujasiliamali wakifuatilia mada wakati kufungwa kwa mafunzo ya Ujasiliamali.Pichana na Mr.PENGO -MMG-Mbeya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...