Na Jonas Kamaleki, Paris 

Tanzania yapongezwa katika Utawala bora kwa kuwa na sheria YA Haki YA kupata Taarifa ambayo utasaidia kupunguza vitendo vya rushwa.

 Pongezi hizo zimetolewa leo jijini Paris, Ufaransa wakati wa Mkutano wa Kilele kuhusu Mpango wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) na Mkurugenzi wa Asasi za Kiraia na Ushirikishwaji wa OGP, Bw. Paul Maassen. 
"Haki ya kupata taarifa ni kati ya mihimili muhimu katika kudondokana na vitendo vya rushwa kama ilivyofanya Tanzania na Kenya," alisema Maassen. Amezitaka nchi nyingine ambazo hazijafanya hivyo kuhakikisha zinakuwa na sheria za namna hiyo ili kuongea uwazi katika shughuli za Serikali. 
Naye Mtafiti wa masuala ya Habari, Bi Alina Mungiu amesema nchi zilizo na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa zinafanya vizuri katika kusambaza na rushwa na ufisadi. Amesema hayo wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha Asasi za Kiraia hapa jijini Paris kuhusu ulimwengu wa kidigitali. 
Bi Mungiu amesema kuwa Serikali inabidi kufanya shughuli zake kwa uwazi zaidi kwa kutumia Serikali Mtandao (e-government). Aliongeza kuwa Maadili katika jamii ni jambo la kushirikiana baina ya Serikali na wananchi na si suala la Serikali peke yake. 
Kwa kufanya hivyo malalamiko ya wananchi kwa viongozi wao yatapungua. " Wananchi wanapaswa kuwa na maamuzi katika mambo yanayowahusu na si kusubiri kuletewa na Serikali," alisisitiza Mungiu.
Mkutano huu wa Kilele umefunguliwa na Rais wa Ufaransa, Francois Hollande na kuhudhuriwa na Viongozi wa nchi zaidi ya 13 akiwemo Rais Barrack Obama na Waziri Mkuu wa Canada ambao wameshriki kwa njia ya video. 

Suala la msingi linalojadiliwa ni kuhusu uwazi katika kuendesha shughuli za Serikali ambapo Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha Dhamira ya dhati ya kuendesha shughuli zake kwa uwazi ikiwemo kusambaza na rushwa
 Mkurugenzi wa Ushirikishwaji wa Asasi za Kiraia Bw. Paul Maasen akiongea na washiriki wa mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alisema serikali kutoa huduma kwa uwazi kutasaidia kuondoa vitendo vya rushwa na uwazi.
Mtafiti katika masuala ya habari Bi. Alina Mungiu (wakwanza kulia)akijibu maswali wakati wa kikao cha Asasi za Kiraia katika mkutano wa Nne wa Mpango wa uendeshaji wa serikali kwa uwazi Jijini Paris Nchini Ufaransa ambapo alieleza jinsi uwepo za sheria za habari na sheria za haki ya kupata taarifa zinavyoweza kusaidia katika mapambano dhidi ya rushwa. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO-PARIS 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...