Na Anthon John Globu ya jamii.
IKIWA
imesalia siku moja kufikia maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad
Kiongozi wa waislam wa madhebu ya shia Ithnashariya Tanzania Shekhe
Hemed Jalala amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuhurumiana hasa
wenye uwezo kuwahurumia wasio na uwezo.
Akizungumza
na waandishi wahabari Leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es
salaam amesema Mtume Mohammad alifundisha kuwa dini imekuja kutunza
Upendo na amani hivyo ni vyema waTanzania kuishi kwa Upendo bila kujali
utofauti wa dini zao.
"Mtu
kupenda nchi ni katika amani na pia dini imekuja kutunza upando na
amani watanzania tusibaguane kutokana na dini zetu" amesema Jalala.
Hata
Hivyo Sheikh Hemed amebainisha kuwa ni vyema jamii kuyaishi maisha
aliyoishi Mtume Mohammad ikiwa ni pamoja na sifa kuumbili alizokuwa nazo
Mtume ambazo nikuwa mkweli na mwaminifu.
Sambamba
na hayo ameongeza kuwa Kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na watanzania
hasa kwa kipindi hiki chakukumbukwa kwa kuzaliwa kwa Mtume ni kuishi kwa
amani na ushirikiano kwa kuwa vitabu vyote vya dini vimekuja
kuunganisha watu.
Shekhe Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari kueleka maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mtume ( S.A.W), kulia ni mlezi wa Hauzat Imamu Swadiq Mzee Rashidi Mashtog na upande wa kushoto ni Naibu kiongozi Mkuu Mohammad Abdi .
Shekhe Hemed Jalala akizungumza na waandishi wa habari kueleka maadhimisho ya Siku ya kuzaliwa Mtume ( S.A.W), kulia ni mlezi wa Hauzat Imamu Swadiq Mzee Rashidi Mashtog na upande wa kushoto ni Naibu kiongozi Mkuu Mohammad Abdi .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...