Na Biseko Lisso Ibrahim WUUM (U)

Kampuni ya Huduma ya Meli (MSCL) imesema meli yake ya MV Clarias itarejesha safari zake za kila siku kutoka Bandari ya Mwanza kwenda visiwa vya Ukerewe baada ya ukarabati mkubwa kukamilika mwishoni mwa wiki hii.

Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), mara baada ya kukagua meli hiyo Kaimu Mtendaji Mkuu wa MSCL, Bw. Eric Hamisi amesema meli hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 295 kwa safari moja ukarabati wake umefikia hatua za mwisho na umetumia fedha za ndani kiasi cha shilingi milioni 20.

“Kwa muda mrefu meli zetu zimesimama kutoa huduma kwa sababu ya kukosa fedha za ukarabati, hivyo tumeweka mkakati wa muda mfupi ambapo tumeweza kukusanya fedha za madeni na tumekuja na mkakati wakudhibiti mapato ili tuweze kujiengea uwezo na kufanya ukarabati kwa meli ambazo zilikuwa zimaharibika na kukaa tu”, amesema Hamis.

Ameongeza kuwa kwa sasa pamoja na mpango wa ukarabati wa meli hizo Kampuni iko kwenye hatua za mwisho kuboresha mifumo ya kukatisha tiketi za meli zake zote kutoka kwenye njia ya kawaida na kwenda njia ya ya kielektorniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

“Kwa sasa tunakamilisha utaratibu wa manunuzi ili kupata mzabuni atakayetupa huduma za ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektoroniki ili kuweza kudhibiti mapato yanayopotea kwa kutumia njia za kawaida”, alisisitiza Bw. Hamis.

Bw. Hamis ametanabaisha kuwa hatua za kumpata mzabuni wa kujenga meli mpya moja katika Ziwa Viktoria ipo katika hatua za mwisho ambapo meli hiyo ikikamilika itarahisisha usafiri katika maeneo ya Kanda ya Ziwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho amesema kuwa Serikali kwa sasa inashughulikia suala la mishahara ili kuimairisha utendaji wa kampuni hiyo.Aidha, amewataka kuhakikisha wanadhibiti mianya yote ya mapato ili kuhakikisha Kampuni inatumia fedha zake za ndani katika ukarabati wa meli zake.

Kampuni ya MSCL iko kwenye mpango mkakati wa muda mfupi ambao unaishia mwezi Aprili mwaka huu ambapo pamoja na kuboresha mifumo mbalimbali imejipanga kukarabati Meli nne ambazo ni MV clarias, MV Serengeti, MT. Sangara na ML Wimbi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...