Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiomba Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika mkakati wake wa kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.

Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi ya AfDB waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Prof. Mbarawa ameishukuru benki hiyo kwa ushirikiano inaoipa Serikali ya Tanzania katika miradi mingi ya ujenzi wa barabara na kuiomba kuiunga mkono katika uwekezaji mkubwa inaoufanya katika miradi ya usafiri wa anga na reli.

“Tumejipanga kukuza uchumi kwa kuimarisha sekta za barabara,anga,reli na bandari hivyo tunaomba ushirikiano wenu kadri tunavyouhitaji ili kufikia malengo yetu kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara ambayo Tanzania imenufaika na AfDB kuwa ni barabara ya Kibondo-Kasulu-Manyovu Km 250, Makutano-Nata-Mugumu-Mto wa Mbu hadi Loliondo Km 213, Makurunge-Saadani-Pangani-Tanga KM 178 na barabara za pete jijini Dar es Salaam Km 34.

“Kuimarika kwa Sekta ya miundombinu nchini hasa sekta ya anga, reli na barabara, kutaimarisha sekta za utalii na kilimo na hivyo kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye mjumbe wa Bodi ya AfDB Dkt. Weggoro Nyamajeje Calleb amezungumzia umuhimu wa miradi ya ujenzi inayoanzishwa hapa nchini kutoa fursa za ajira kwa wananchi na kuwekewa mazingira endelevu ili ilete mabadiliko chanya katika maisha ya watu na taifa kwa ujumla.

Dkt. Calleb amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ili kuiwezesha nchi kuwa na miundombinu bora na yakutosha na hivyo kuchochea maendeleo.

Ujumbe wa AfDB upo hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine leo umepata fursa ya kubadilishana uzoefu na viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili kujua mikakati yake katika kuboresha miundombinu hapa nchini na namna inavyoweza kutoa ushirikiano katika kuiwezesha.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza kwa makini mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), Bi, Lekhethe Mmakgoshi (wa pili kushoto), wakati alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza kwa makini mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), Bi, Lekhethe Mmakgoshi (wa pili kushoto), wakati alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto ), akifafanua jambo kwa wajumbe wa  Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), bi, Lekhethe Mmakgoshi, Dkt. Weggoro Nyamajeje na Dkt. Bright Okogu (wa kwanza kulia), alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB) walipokutana Jijini Dar es salaam leo.Imetolewa Na Kitengo cha Habari Na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...