o   Zaidi ya wanawake 580 wajawazito na watoto wachanga  waokolewa
o   Zaidi ya wakina mama 6,000 wapatiwa elimu ya afya kila kaya
o   Mradi warahisishwa na Huduma ya M-Pesa ya Vodacom
 Wakina mama wajawazito na watoto wa wilayani Sengerema wamefarijika baada ya kujionea manufaa ya mradi wa kutokomeza vifo vya akina mama hao na watoto wachanga ukiendelea vizuri na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii yao inayowazunguka,Mradi huo ambao ulizinduliwa mwaka jana wilayani humo  chini ya ufadhili wa taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kushirikiana na  mashirika ya kimataifa ya USAID, Path Finder na Touch Foundation unazidi kuleta mafanikio makubwa katika wilya hiyo.
 Moja ya mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kupitia mradi huu ni kuokoa maisha ya wanawake wajawazito na watoto wachanga wapatao 580pia umewezesha mafunzo  kwa wahudumu wa Afya wa ngazi ya Jamii wanaopita kila kaya kutoa elimu, ili kubadili mitazamo hasi ya baadhi ya akina mama kutofika kwenye vituo vya afya kupatiwa huduma za uzazi na akina mama zaidi ya 6,000 wamepatiwa elimu hii.
Wafadhili wa mradi huu  wamekuwa wakigharamia mafunzo kwa wahudumu wa afya na usafiri wa akina mama wajawazito wanaokaribia kujifungua kuwawahisha kwenye vituo vya afya kupata matibabu ya haraka pindi panapohitajika msaada ambapo wameingia mkataba maalumu na madereva wa teksi katika kufanikisha mradi huu ambao hutoa huduma hii kwa haraka na kulipwa  kupitia huduma ya M-Pesa.

 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dk.Hamis Kingwangalla, Akiongea na wakazi wa wilaya ya Sengerema wakati wa Uzinduzi wa mradi huu.       

Wakina mama wajawazito na watoto wa wilayani Sengerema wamefarijika baada ya kujionea manufaa ya mradi wa kutokomeza vifo vya akina mama hao na watoto wachanga ukiendelea vizuri na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii yao inayowazunguka. Habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...