Na
Bashir Yakub .
Ni kweli ardhi umenunua
kwa hela yako, ni kweli kiwanja umetafuta
mwenyewe, ni kweli wewe ni Mtanzania
wala sio mgeni, lakini
pia ni kweli
ukubali kuwa ardhi
hiyo unaimiliki katika
kipindi maalum na
sio moja kwa
moja/milele.
Hapo ulipo
unapoita nyumbani kwako
unapamiliki kwa muda
maalum na sio moja
kwa moja kama
unavyodhani. Tanzania hakuna anayemiliki
ardhi moja kwa
moja bali wote
tunamiliki kwa muda
maalum.
Hati ya kumiliki
ardhi uliyonayo au unayotafuta
kupata hutolewa kwa
muda maalum. Hakuna hati
ya milele isipokuwa
kila hati inacho
kipindi chake.
Kipindi
kinapoisha maana yake
na umiliki wako umeisha.
Tutaona ufanye
nini kipindi kinapoisha na athari za kuacha
kufanya ulichotakiwa kufanya baada
ya kipindi kuisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...