Frank Mvungi-Maelezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepongezwa kwa kuiwezeshaTaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya upasuaji wa kihistoria tangu kuanzishwa kwake.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangassa wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai nchini India waliosaidia kufanikisha upasuaji huo wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) kwenye moyo .

Upasuaji huu uliwahusisha madaktari 6 toka Hospitali ya Saifee umesaidia kuwaongezea ujuzi wataalamu wa Taasisi hiyo na kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuwasafirisha nje wagonjwa ili waweze kupata matibabu.

“Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nchini India Serikali ingelipia zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kama gharama za matibabu” Alisisitiza Dkt. Nyangassa. “

Akizungumzia upasuaji mwingine uliofanyika kwa wagonjwa 8 Dkt. Nyangassa amesema kuwa ni upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo kwa kuibadilisha. 
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala. 
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akifafanua jambombele ya waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Machi katika Taasisi hiyo ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Madhebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upandikizaji wa Mishipa kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai, India Dkt. Yunus Loya. 
Daktari Bingwa wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Yunus Loya akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa (kulia). 
Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kuzibua njia mbili, Athumani Waziri akielezea namna alivyofarijika baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktari hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...